11. Mtu apataye mali isiyo halalini kama kware akusanyaye makinda ambayo hakuyaangua:Wakati wa kilele cha ujana wake itamchopoka,na mwishoni atakuwa mtu mpumbavu.
12. Kuna kiti cha enzi kitukufukiti kilichoinuliwa juu;huko ndiko mahali petu patakatifu.
13. Ee Mwenyezi-Mungu tumaini la Israeli,wote wanaokukataa wataaibishwa;wanaokuacha wewe watatoweka,kama majina yaliyoandikwa vumbini,kwa maana wamekuacha wewe Mwenyezi-Mungu,uliye chemchemi ya maji ya uhai.
14. Uniponye, ee Mwenyezi-Mungu, nami nitapona;uniokoe, nami nitaokoka;maana, wewe ndiwe sifa yangu.
15. Tazama watu wanavyoniambia:“Jambo alilotishia Mwenyezi-Mungu liko wapi?Acha basi lije!”
16. Sikuikimbia huduma yako ya kuwa mchungajiwala sikutamani ile siku ya maafa ije.Wewe mwenyewe wajua nilichosema kwa mdomo wangu,nilichotamka wakijua waziwazi.