Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya watu hawa:“Kweli wamependa sana kutangatanga,wala hawakujizuia;kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu siwapokei.Sasa nitayakumbuka makosa yao,na kuwaadhibu kwa dhambi zao.”