23. Najua, ee Mwenyezi-Mungu,binadamu hana uwezo na maisha yake;hakuna mtu awezaye kuyaongoza maisha yake.
24. Utukosoe, ee Mwenyezi-Mungu, lakini si kwa ghadhabu,wala kwa hasira yako, tusije tukaangamia.
25. Imwage hasira yako juu ya mataifa yasiyokuabudu,na juu ya watu ambao hawakutambui.Maana, wamewaua wazawa wa Yakobo;wamewaua na kuwaangamiza kabisa,na nchi yao wameiacha magofu.