Wimbo Ulio Bora 1:14-17 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Mpenzi wangu ni kama maua ya hina yachanuayo,kwenye mashamba ya mizabibu huko Engedi.

15. Hakika u mzuri, ee mpenzi wangu,hakika u mzuri!Macho yako ni kama ya hua!

16. Hakika u mzuri ewe nikupendaye,u mzuri kweli!Majani mabichi yatakuwa kitanda chetu;

17. mierezi itakuwa nguzo za nyumba yetu,na miberoshi itakuwa dari yake.

Wimbo Ulio Bora 1