Walawi 24:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

2. “Waamuru watu wa Israeli wakuletee mafuta safi kwa ajili ya taa ili taa hiyo iendelee kuwaka daima.

3. Aroni ataiweka taa hiyo ndani ya hema la mkutano, nje ya pazia la sanduku la maamuzi ili ipate kuwaka mbele yangu tangu usiku mpaka asubuhi. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu.

Walawi 24