7. Kuhani atamtolea mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumfanyia huyo mama ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu. Hivyo huyo mwanamke atakuwa safi kutokana na damu yake. Huo ni mwongozo kuhusu mwanamke yeyote anayejifungua mtoto wa kiume au wa kike.
8. “Kama hawezi kutoa mwanakondoo, basi, ataleta hua wawili au makinda mawili ya njiwa; mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuondolea dhambi. Kuhani atamfanyia mama huyo ibada ya upatanisho, naye atakuwa safi.”