Waebrania 3:17-19 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arubaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.

18. Mungu alipoapa: “Hawataingia mahali pangu pa pumziko,” alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.

19. Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.

Waebrania 3