Waebrania 1:7-14 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Lakini kuhusu malaika, alisema:“Amewafanya malaika wake kuwa upepo,na wahudumu wake ndimi za moto.”

8. Lakini kuhusu Mwana, Mungu alisema:“Kiti chako cha enzi, ee Mungu, chadumu milele na milele!Wewe wawatawala watu wako kwa haki.

9. Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu.Ndiyo maana Mungu, Mungu wako, amekuweka wakfuna kukumiminia furaha kubwa kuliko wenzako.”

10. Na tena:“Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo,mbingu ni kazi ya mikono yako.

11. Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima,zote zitachakaa kama vazi.

12. Utazikunjakunja kama koti,nazo zitabadilishwa kama vazi.Lakini wewe ni yuleyule daima,na maisha yako hayatakoma.”

13. Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake:“Keti upande wangu wa kulia,mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.”

14. Malaika ni nini ila roho wanaomtumikia Mungu na ambao hutumwa kuwasaidia wale watakaopokea wokovu?

Waebrania 1