Waamuzi 10:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Baada ya kifo cha Abimeleki, Tola mwana wa Pua mwana wa Dodo, wa kabila la Isakari, akatokea kuwakomboa Waisraeli. Tola aliishi Shamiri katika nchi ya milima ya Efraimu.

2. Alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini na mitatu, kisha akafariki na kuzikwa huko Shamiri.

Waamuzi 10