4. Mji wa Gaza utahamwa,Ashkeloni utakuwa tupu.Wakazi wa Ashdodi watatimuliwa mchana,na wale wa Ekroni watang'olewa.
5. Ole wenu wakazi wa nchi za pwani,watu mnaoishi huko Krete!Mwenyezi-Mungu ametamka dhidi yenuenyi wakazi wa Kanaani, nchi ya Filistia:Mimi nitawaangamiza asibaki hata mkazi mmoja!
6. Nanyi nchi za pwani mtafanywa kuwa malisho;mtakuwa vibanda vya wachungajina mazizi ya kondoo.
7. Nchi ya pwani itamilikiwa na mabaki ya ukoo wa Yuda.Watachunga mifugo yao huko.Nyumba za mji wa Ashkelonizitakuwa mahali pao pa kulala.Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wao atawakumbukana kuwarudishia hali yao njema.
8. “Nimeyasikia masuto ya Moabuna dhihaka za Waamoni;jinsi walivyowasuta watu wangu,na kujigamba kuiteka nchi yao.
9. Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,mimi Mungu wa Israeli,Moabu itakuwa kama Sodomana Amoni itakuwa kama Gomora.Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi,zitakuwa ukiwa milele.Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara,watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.”