Obadia 1:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Siku ile mlisimama kando mkitazama tu,wakati wageni walipopora utajiri wao,naam, wageni walipoingia malango yaona kugawana utajiri wa Yerusalemu kwa kura.Kwa hiyo nanyi mlitenda kama wazawa wao.

12. Msingalifurahia siku hiyo ndugu zenu walipokumbwa na mikasa;msingaliwacheka Wayudana kuona fahari wakati walipoangamizwa;msingalijigamba wenzenu walipokuwa wanataabika.

13. Msingeliingia katika mji wa watu wangu,siku walipokumbwa na maafa;msingelipora mali zao, siku hiyo ya maafa yao.

14. Msingelisimama kwenye njia pandana kuwakamata wakimbizi wao;wala msingeliwakabidhi kwa adui zaowale waliobaki hai.

15. “Siku inakaribia ambapo mimi Mwenyezi-Mungunitayahukumu mataifa yote.Kama mlivyowatendea wengine, ndivyo mtakavyotendewa,mtalipwa kulingana na matendo yenu.

16. Maana, kama walivyokunywa kikombe cha ghadhabu yangukwenye mlima wangu mtakatifundivyo na mataifa jirani yatakavyokunywa;watakunywa na kupepesuka,wataangamia kana kwamba hawakuwahi kuwapo duniani.

17. “Lakini mlimani Siyoni watakuwapo wale waliosalimikanao utakuwa mlima mtakatifu.Wazawa wa Yakobo wataimiliki tena nchi iliyokuwa yao.

Obadia 1