Wale waliokuwa uhamishoni kule Babuloni, walirudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda, kila mmoja akarudi mjini kwake. Jamaa zao walikuwa wamekaa Babuloni tangu mfalme Nebukadneza alipowahamishia huko wakiwa mateka.