2. Sanbalati na Geshemu walituma ujumbe kwangu wakisema, “Na tukutane kwenye kijiji kimojawapo cha tambarare ya Ono.” Lakini walikusudia kunidhuru.
3. Basi, nikawapelekea wajumbe, nikisema, “Kazi ninayoifanya ni muhimu sana. Hivyo siwezi kuja kwenu ili kazi isije ikasimama.”
4. Waliendelea kunitaka niende kwao mara nne, lakini nikawapa jibu lilelile.
5. Mara ya tano, Sanbalati akanitumia barua ya hadhara kwa njia ya mjumbe wake.