Nehemia 11:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha, viongozi wa watu wakakaa mjini Yerusalemu; watu wengine wote, wakapiga kura kati ya kila jamaa kumi ili kuchagua jamaa moja itakayokaa mjini Yerusalemu, mji mtakatifu. Jamaa nyingine tisa zikakaa katika miji yao mingine.

2. Watu wakawasifu wale wote waliokubali kukaa mjini Yerusalemu.

Nehemia 11