Mwanzo 50:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hapo Yosefu akamkumbatia baba yake akilia na kumbusu.

2. Kisha, akawaagiza waganga wake wampake Israeli, baba yake, dawa ili asioze, nao wakafanya hivyo.

3. Kama kawaida, siku arubaini zilihitajika kwa kazi hiyo. Wamisri nao wakaomboleza kifo cha Yakobo kwa muda wa siku sabini.

Mwanzo 50