Mwanzo 5:3-9 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Adamu alipokuwa na umri wa miaka 130, alipata mtoto aliyefanana naye, na mwenye sura kama yake; akamwita Sethi.

4. Baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

5. Adamu alifariki akiwa na umri wa miaka 930.

6. Sethi alipokuwa na umri wa miaka 105, alimzaa Enoshi.

7. Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

8. Sethi alifariki akiwa na umri wa miaka 912.

9. Enoshi alipokuwa na umri wa miaka 90, alimzaa Kenani.

Mwanzo 5