Mwanzo 5:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ifuatayo ni orodha ya wazawa wa Adamu. Wakati Mungu alipomuumba binadamu, alimuumba kwa mfano wake.

2. Aliwaumba mwanamume na mwanamke, kisha akawabariki na kuwapa jina “Binadamu.”

3. Adamu alipokuwa na umri wa miaka 130, alipata mtoto aliyefanana naye, na mwenye sura kama yake; akamwita Sethi.

Mwanzo 5