Mwanzo 49:26-32 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Baraka za baba yako zishinde baraka za milima ya milele,ziwe bora kuliko vilima vya kale.Baraka hizo na ziwe juu ya kichwa cha Yosefu,juu ya paji lake yeye aliyekuwa ametengwa na ndugu zake.

27. “Benyamini ni mbwamwitu mkali;asubuhi hula mawindo yake,na jioni hugawa nyara.”

28. Hayo ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hayo ndiyo maneno aliyowaambia baba yao alipowabariki, kila mmoja wao kama alivyostahili.

29. Kisha Israeli akawaagiza wanawe hivi, “Mimi karibu nife na kujiunga na watu wangu. Nizikeni pamoja na wazee wangu katika pango lililoko shambani mwa Efroni Mhiti,

30. kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia.

31. Huko ndiko walikozikwa Abrahamu na mkewe Sara; huko ndiko walikozikwa Isaka na mkewe Rebeka; na huko ndiko nilikomzika Lea.

32. Shamba hilo na pango lake lilinunuliwa kwa Wahiti.”

Mwanzo 49