Mwanzo 49:12-20 Biblia Habari Njema (BHN)

12. “Macho yake ni mekundu kwa divai,meno yake ni meupe kwa maziwa.

13. “Zebuluni ataishi sehemu za pwani,pwani yake itakuwa mahali pa kuegesha meli.Nchi yake itapakana na Sidoni.

14. “Isakari ni kama punda mwenye nguvu,ajilazaye kati ya mizigo yake.

15. “Aliona kuwa mahali pa kupumzikia ni pema,na kwamba nchi ni ya kupendeza,akauinamisha mgongo wake kubeba mzigo,akawa mtumwa kufanya kazi za shuruti.

16. “Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake,kama mojawapo ya makabila ya Israeli.

17. “Atakuwa kama nyoka njiani,nyoka mwenye sumu kando ya njia,aumaye visigino vya farasi,naye mpandafarasi huanguka chali.

18. “Ee Mwenyezi-Mungu, nangojea uniokoe!

19. “Gadi atashambuliwa na wanyanganyi,lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia.

20. “Ardhi ya Asheri itatoa mavuno kwa wingi,naye atatoa chakula kimfaacho mfalme.

Mwanzo 49