8. Wazawa wa Israeli ambao walikwenda Misri pamoja naye walikuwa Reubeni, mzaliwa wake wa kwanza,
9. pamoja na wana wa Reubeni: Henoki, Palu, Hesroni na Karmi.
10. Simeoni na wanawe: Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli, aliyezaliwa na mwanamke Mkanaani.
11. Lawi na wanawe: Gershoni, Kohathi na Merari.
12. Yuda na wanawe: Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera. (Lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli.
13. Isakari na wanawe: Tola, Puva, Yashubu na Shimroni.