1. Wafuatao ni wazawa wa Esau (yaani Edomu).
2. Esau alioa wake Wakanaani: Ada binti Eloni Mhiti, Oholibama binti Ana, binti Sibeoni, Mhivi,
3. na Basemathi, binti Ishmaeli, dada yake Nebayothi.
4. Ada alimzalia Esau Elifazi, naye Basemathi akamzalia Reueli.
5. Oholibama alimzalia Yeushi, Yalamu na Kora. Hao ndio watoto wa kiume wa Esau ambao wake zake walimzalia alipokaa katika nchi ya Kanaani.