24. Watoto wa kiume wa Raheli walikuwa Yosefu na Benyamini.
25. Watoto wa kiume waliozaliwa na Bilha, mjakazi wa Raheli, walikuwa Dani na Naftali.
26. Na watoto wa kiume waliozaliwa na Zilpa, mjakazi wa Lea, walikuwa Gadi na Asheri. Hao ndio watoto wa kiume wa Yakobo, aliowazaa alipokuwa kule Padan-aramu.
27. Yakobo aliondoka akaenda Mamre kwa baba yake Isaka, huko Kiriath-arba, yaani Hebroni, mahali ambapo Abrahamu na Isaka walikaa kama wageni.
28. Isaka alikuwa na miaka 180
29. akafariki akiwa mzee wa miaka mingi. Watoto wake, Esau na Yakobo wakamzika.