Mwanzo 3:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini walioumbwa na Mwenyezi-Mungu. Basi, nyoka akamwambia huyo mwanamke, “Ati Mungu alisema msile matunda ya mti wowote bustanini?”

2. Mwanamke akamjibu huyo nyoka, “Twaweza kula matunda ya mti wowote bustanini;

3. lakini Mungu alisema, ‘Msile matunda ya mti ulio katikati ya bustani, wala msiuguse, msije mkafa.’”

4. Nyoka akamwambia mwanamke, “Hamtakufa!

5. Mungu alisema hivyo kwa sababu anajua kwamba mkila matunda ya mti huo mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

Mwanzo 3