Mwanzo 17:20-27 Biblia Habari Njema (BHN)

20. “Na, kuhusu Ishmaeli, nimesikia ombi lako. Nitambariki, nitamjalia watoto wengi na kuwazidisha sana. Ishmaeli atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya kuwa baba wa taifa kubwa.

21. Lakini agano langu litathibitika kwa Isaka ambaye Sara atakuzalia mwakani wakati kama huu.”

22. Basi, Mungu alipomaliza kuongea, akamwacha Abrahamu.

23. Kisha, siku hiyohiyo, Abrahamu akamtahiri mwanawe Ishmaeli na kuwatahiri watumwa wote wa kiume waliozaliwa nyumbani mwake na walionunuliwa kwa fedha zake, kama Mungu alivyomwamuru.

24. Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 99 alipotahiriwa.

25. Na Ishmaeli mwanawe alikuwa na umri wa miaka 13 alipotahiriwa.

26. Abrahamu na mwanawe Ishmaeli

27. pamoja na wanaume wote wa nyumba yake, watumwa wote waliozaliwa nyumbani mwake na walionunuliwa kwa fedha zake walitahiriwa siku hiyohiyo.

Mwanzo 17