1. Wakati Abramu alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Mwenyezi-Mungu alimtokea, akamwambia, “Mimi ni Mungu mwenye nguvu. Fuata mwongozo wangu na kuishi bila lawama.
2. Nami nitafanya agano nawe na kuwazidisha wazawa wako.”
3. Hapo Abramu akasujudu. Naye Mungu akamwambia,
4. “Ninafanya agano hili nawe: Utakuwa baba wa mataifa mengi.
5. Tangu sasa, hutaitwa tena Abramu, bali utaitwa Abrahamu, maana nimekufanya kuwa baba wa mataifa mengi.
6. Nitakufanya uwe na wazawa wengi sana; kwako nitazusha mataifa mengi na wafalme.