6. Watoto wa kiume wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani.
7. Watoto wa kiume wa Kushi walikuwa Seba, Hawila, Sabta, Raama na Sabteka. Watoto wa kiume wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.
8. Kushi alikuwa baba yake Nimrodi ambaye alikuwa shujaa wa kwanza duniani.
9. Alikuwa mwindaji shujaa mbele ya Mwenyezi-Mungu, ndiyo maana kuna msemo usemao, “Kama Nimrodi mwindaji shujaa mbele ya Mwenyezi-Mungu.”
10. Miji ya kwanza ya utawala wake ilikuwa Babuloni, Ereki na Akadi, katika nchi ya Shinari.