3. Binadamu hufaidi ninikwa jasho lake lote hapa duniani?
4. Kizazi chapita na kingine chaja,lakini dunia yadumu daima.
5. Jua lachomoza na kutua;laharakisha kwenda machweoni.
6. Upepo wavuma kusini,wazunguka hadi kaskazini.Wavuma na kuvuma tena,warudia mzunguko wake daima.
7. Mito yote hutiririkia baharini,lakini bahari kamwe haijai;huko ambako mito hutiririkiandiko huko inakotoka tena.
8. Mambo yote husababisha uchovu,uchovu mkubwa usioelezeka.Jicho halichoki kuona,wala sikio kusikia.
9. Yaliyokuwako ndio yatakayokuwako,yaliyotendeka ndio yatakayotendeka;duniani hakuna jambo jipya.
10. Watu husema, “Tazama jambo jipya,”kumbe lilikwisha kuwako zama za kale.