33. Sikilizeni mafunzo mpate hekima,wala msiyakatae.
34. Heri mtu anayenisikiliza,anayekaa kila siku mlangoni pangu,anayekesha karibu na milango yangu.
35. Anayenipata mimi amepata uhai,amepata upendeleo kwa Mwenyezi-Mungu.
36. Asiyenipata anajidhuru mwenyewe;wote wanaonichukia wanapenda kifo.”