Methali 8:19-29 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Matunda yangu ni mazuri kuliko dhahabu safi,faida yangu yashinda ile ya fedha bora.

20. Natembea katika njia ya uadilifu;ninafuata njia za haki.

21. Mimi huwatajirisha wanaonipenda,huzijaza tele hazina zao wanipendao.

22. “Mwenyezi-Mungu aliniumba mwanzoni mwa kazi yake,zama za zama kabla ya kuwako kitu chochote.

23. Nilifanywa mwanzoni mwa nyakati,nilikuwako kabla ya dunia kuanza.

24. Nilizaliwa kabla ya vilindi vya bahari,kabla ya chemchemi zibubujikazo maji.

25. Kabla ya milima haijaumbwa,na vilima kusimamishwa mahali pake,mimi nilikuwako tayari.

26. Kabla Mungu hajaumba dunia na mashamba yake,wala chembe za kwanza za mavumbi ya dunia.

27. Nilikuwako wakati alipoziweka mbingu,wakati alipopiga duara juu ya bahari;

28. wakati alipoimarisha mawingu mbinguni,alipozifanya imara chemchemi za bahari;

29. wakati alipoiwekea bahari mpaka wake,maji yake yasije yakavunja amri yake;wakati alipoiweka misingi ya dunia.

Methali 8