16. Kwa msaada wangu viongozi hutawala,wakuu na watawala halali.
17. Nawapenda wale wanaonipenda;wanaonitafuta kwa bidii hunipata.
18. Utajiri na heshima viko kwangu,mali ya kudumu na fanaka.
19. Matunda yangu ni mazuri kuliko dhahabu safi,faida yangu yashinda ile ya fedha bora.
20. Natembea katika njia ya uadilifu;ninafuata njia za haki.
21. Mimi huwatajirisha wanaonipenda,huzijaza tele hazina zao wanipendao.
22. “Mwenyezi-Mungu aliniumba mwanzoni mwa kazi yake,zama za zama kabla ya kuwako kitu chochote.
23. Nilifanywa mwanzoni mwa nyakati,nilikuwako kabla ya dunia kuanza.
24. Nilizaliwa kabla ya vilindi vya bahari,kabla ya chemchemi zibubujikazo maji.