Methali 8:13-25 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni kuchukia uovu.Nachukia kiburi, majivuno na maisha mabaya;nachukia na lugha mbaya.

14. Nina uwezo wa kushauri na nina hekima.Ninao ujuzi na nina nguvu.

15. Kwa msaada wangu wafalme hutawala,watawala huamua yaliyo ya haki.

16. Kwa msaada wangu viongozi hutawala,wakuu na watawala halali.

17. Nawapenda wale wanaonipenda;wanaonitafuta kwa bidii hunipata.

18. Utajiri na heshima viko kwangu,mali ya kudumu na fanaka.

19. Matunda yangu ni mazuri kuliko dhahabu safi,faida yangu yashinda ile ya fedha bora.

20. Natembea katika njia ya uadilifu;ninafuata njia za haki.

21. Mimi huwatajirisha wanaonipenda,huzijaza tele hazina zao wanipendao.

22. “Mwenyezi-Mungu aliniumba mwanzoni mwa kazi yake,zama za zama kabla ya kuwako kitu chochote.

23. Nilifanywa mwanzoni mwa nyakati,nilikuwako kabla ya dunia kuanza.

24. Nilizaliwa kabla ya vilindi vya bahari,kabla ya chemchemi zibubujikazo maji.

25. Kabla ya milima haijaumbwa,na vilima kusimamishwa mahali pake,mimi nilikuwako tayari.

Methali 8