Methali 8:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sikilizeni! Hekima anaita!Busara anapaza sauti yake!

2. Juu penye mwinuko karibu na njia,katika njia panda ndipo alipojiweka.

3. Karibu na malango ya kuingilia mjini,mahali wanapoingia watu anaita kwa sauti:

4. “Enyi watu wote, nawaita nyinyi!Wito wangu ni kwa ajili ya binadamu.

5. Enyi wajinga, jifunzeni kuwa na akili;sikilizeni kwa makini enyi wapumbavu.

6. Sikilizeni maana nitakachosema ni jambo muhimu;midomoni mwangu mtatoka mambo ya adili.

7. Kinywa changu kitatamka kweli tupu;uovu ni chukizo midomoni mwangu.

8. Kinywa changu kitatamka maneno ya kweli,udanganyifu ni haramu midomoni mwangu.

9. Kwa mtu mwelewa kila kitu ni wazi,kwa mwenye maarifa yote ni sawa.

10. Chagua mafundisho yangu badala ya fedha;na maarifa badala ya dhahabu safi.

11. “Mimi Hekima nina thamani kuliko johari;chochote unachotamani hakiwezi kulingana nami.

12. Mimi Hekima ninao ujuzi;ninayo maarifa na busara.

13. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni kuchukia uovu.Nachukia kiburi, majivuno na maisha mabaya;nachukia na lugha mbaya.

Methali 8