14. “Ilinilazimu kutoa tambiko zangu;leo hii nimekamilisha nadhiri yangu.
15. Ndio maana nimetoka ili nikulaki,nimekutafuta kwa hamu nikakupata.
16. Nimetandika kitanda changu vizuri,kwa shuka za rangi za kitani kutoka Misri.
17. Nimekitia manukato, manemane, udi na mdalasini.
18. Njoo tulale pamoja mpaka asubuhi;njoo tujifurahishe kwa mahaba.
19. Mume wangu hayumo nyumbani,amekwenda safari ya mbali.
20. Amechukua bunda la fedha;hatarejea nyumbani karibuni.”
21. Alimshawishi kwa maneno mengi ya kubembeleza;kijana akashawishika kwa maneno yake matamu.