Methali 7:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Alikuwa mwanamke wa makelele na mkaidi;miguu yake haitulii nyumbani:

12. Mara barabarani, mara sokoni,katika kila kona ya njia hakosekani akivizia.

13. Alimkumbatia kijana huyo na kumbusu,na kwa maneno matamu, akamwambia:

14. “Ilinilazimu kutoa tambiko zangu;leo hii nimekamilisha nadhiri yangu.

15. Ndio maana nimetoka ili nikulaki,nimekutafuta kwa hamu nikakupata.

16. Nimetandika kitanda changu vizuri,kwa shuka za rangi za kitani kutoka Misri.

17. Nimekitia manukato, manemane, udi na mdalasini.

18. Njoo tulale pamoja mpaka asubuhi;njoo tujifurahishe kwa mahaba.

Methali 7