5. Jiokoe kwa kujitoa katika mtego huo,mithili ya paa ama ndege amtorokavyo mwindaji.
6. Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi,fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima.
7. Sisimizi hana kiongozi, ofisa, wala mtawala;
8. lakini hujiwekea chakula wakati wa kiangazi,hujikusanyia akiba wakati wa mavuno.
9. Ewe mvivu, utalala hapo mpaka lini?Utaamka lini katika usingizi wako?
10. Wasema: “Acha nilale kidogo tu,acha nisinzie kidogo!Niache nikunje mikono nipumzike kidogo!”
11. Wakati huo umaskini utakuvamia kama mnyanganyi,ufukara utakufuata kama jambazi.
12. Mtu mwovu, mtu asiyefaa kitu,huzururazurura akisema maneno mapotovu.