32. Mwanamume anayezini na mke wa mtu hana akili kabisa;huyo hujiangamiza yeye mwenyewe.
33. Atapata majeraha na madharau;fedheha atakayopata haitamtoka.
34. Maana wivu wa mume humfanya kuwa mkali kabisa;wakati atakapolipiza kisasi hana cha kuhurumia.
35. Hatakubali fidia yoyote;wala kutulizwa na zawadi zako nyingi.