14. Akiwa amejaa ulaghai moyoni hutunga maovu,huzusha ugomvi kila mahali.
15. Kutokana na hayo maafa yatamvamia ghafla,ghafla atadhurika vibaya asiweze kupona tena.
16. Kuna vitu sita anavyochukia Mwenyezi-Mungu;naam, vitu saba ambavyo ni chukizo kwake:
17. Macho ya kiburi,ulimi mdanganyifu,mikono inayoua wasio na hatia,
18. moyo unaopanga mipango miovu,miguu iliyo mbioni kutenda maovu,
19. shahidi wa uongo abubujikaye uongo,na mtu achocheaye fitina kati ya ndugu.
20. Mwanangu, shika maagizo ya baba yako,wala usisahau mafundisho ya mama yako;
21. yaweke daima moyoni mwako,yafunge shingoni mwako.
22. Yatakuongoza njiani mwako,yatakulinda wakati ulalapo,yatakushauri uwapo macho mchana.
23. Maana amri hiyo ni taa,na sheria hiyo ni mwanga.Maonyo hayo na nidhamu yatuweka njiani mwa uhai.
24. Yatakulinda mbali na mwanamke mbaya,yatakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni.
25. Usimtamani mwanamke huyo kwa uzuri wake,wala usikubali kunaswa kwa kope za macho yake.
26. Mtu hupoteza kipande cha mkate kwa malaya,lakini kwa mke wa mtu mwingine utapoteza uhai wako wote.
27. Je, waweza kuweka moto kifuanina nguo zako zisiungue?
28. Je, waweza kukanyaga makaa ya motona nyayo zako zisiungue?
29. Ndivyo alivyo mwanamume alalaye na mke wa mwenzake;yeyote anayemgusa mwanamke huyo hataacha kuadhibiwa.
30. Watu hawambezi sana mtu akiiba kwa sababu ya njaa;
31. lakini akipatikana lazima alipe mara saba;tena atatoa mali yote aliyo nayo.