Methali 6:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwanangu, kama umejitolea kumdhamini jirani yako,ikiwa umetoa ahadi yako kwa ajili ya mtu huyo,

2. umejibana kwa maneno yako mwenyewe,umejinasa kwa ahadi uliyofanya.

3. Ujue kwamba uko chini ya mamlaka ya mwenzio,lakini mwanangu, ukitaka kujiokoa, basi fanya hivi:Mwendee mtu huyo mara moja umsihi akupe uhuru wako.

4. Jitahidi usiache macho yako yapate usingizi,wala kope za macho yako zisinzie.

5. Jiokoe kwa kujitoa katika mtego huo,mithili ya paa ama ndege amtorokavyo mwindaji.

6. Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi,fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima.

Methali 6