1. Mwanangu, kama umejitolea kumdhamini jirani yako,ikiwa umetoa ahadi yako kwa ajili ya mtu huyo,
2. umejibana kwa maneno yako mwenyewe,umejinasa kwa ahadi uliyofanya.
3. Ujue kwamba uko chini ya mamlaka ya mwenzio,lakini mwanangu, ukitaka kujiokoa, basi fanya hivi:Mwendee mtu huyo mara moja umsihi akupe uhuru wako.
4. Jitahidi usiache macho yako yapate usingizi,wala kope za macho yako zisinzie.
5. Jiokoe kwa kujitoa katika mtego huo,mithili ya paa ama ndege amtorokavyo mwindaji.
6. Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi,fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima.
7. Sisimizi hana kiongozi, ofisa, wala mtawala;
8. lakini hujiwekea chakula wakati wa kiangazi,hujikusanyia akiba wakati wa mavuno.
9. Ewe mvivu, utalala hapo mpaka lini?Utaamka lini katika usingizi wako?
10. Wasema: “Acha nilale kidogo tu,acha nisinzie kidogo!Niache nikunje mikono nipumzike kidogo!”
11. Wakati huo umaskini utakuvamia kama mnyanganyi,ufukara utakufuata kama jambazi.
12. Mtu mwovu, mtu asiyefaa kitu,huzururazurura akisema maneno mapotovu.
13. Hukonyeza jicho kuwakosesha wengine,huparuza kwa nyayo,na kuashiria watu kwa vidole.
14. Akiwa amejaa ulaghai moyoni hutunga maovu,huzusha ugomvi kila mahali.