7. Sasa enyi wanangu, nisikilizeni,wala msisahau maneno ya kinywa changu.
8. Iepushe njia yako mbali naye,wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
9. Usije ukawapa wengine heshima yako,na wakatili miaka yako;
10. wageni wasije wakajishibisha kwa mali yako,na jasho lako likaishia nyumbani kwa mgeni.
11. Mwishoni mwa maisha yako utaombolezawakati mwili wako utakapoangamizwa.
12. Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu,na kudharau maonyo moyoni mwangu!