Methali 4:2-10 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Maana ninawapa maagizo mema,msiyakatae mafundisho yangu.

3. Mimi pia nilikuwa mtoto mwenye baba,nilikuwa mpole, kipenzi cha mama yangu.

4. Baba yangu alinifundisha hiki:“Zingatia kwa moyo maneno yangu,shika amri zangu nawe utaishi.

5. Jipatie hekima, jipatie ufahamu;usisahau wala kupuuza maneno yangu.

6. Usimwache Hekima, naye atakutunza;umpende, naye atakulinda.

7. Jambo la msingi ni kujipatia hekima;toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili.

8. Mthamini sana Hekima, naye atakutukuza;ukimshikilia atakupa heshima.

9. Atakuvika kilemba kizuri kichwani pako,atakupa taji maridadi.”

10. Mwanangu, sikia na kuyapokea maneno yangu,ili upate kuwa na miaka mingi ya kuishi.

Methali 4