15. Iepe njia hiyo wala usiikaribie;jiepushe nayo, uende zako.
16. Waovu kamwe hawalali wasipotenda uovu;hawapati usingizi wasipomkwaza mtu.
17. Maana uovu ndicho chakula chao,ukatili ndiyo divai yao.
18. Njia ya watu wema ni kama nuru ya alfajiri,ambayo hungaa zaidi na zaidi hata mchana kamili.
19. Lakini njia ya waovu ni kama giza nene,hawajui kinachowafanya wajikwae.
20. Mwanangu, sikiliza kwa makini maneno yangu,itegee sikio misemo yangu.
21. Usiyaache yatoweke machoni pako,yahifadhi ndani ya moyo wako.
22. Maana hayo ni uhai kwa mtu anayeyapata,ni dawa kwa mwili wake wote.