Methali 30:29-33 Biblia Habari Njema (BHN)

29. Kuna viumbe vitatu vyenye mwendo wa kupendeza,naam, kuna viumbe vinne vyenye mwendo mzuri;

30. simba: Mnyama mwenye nguvu kuliko wote,wala hamwogopi mnyama mwingine yeyote;

31. jogoo aendaye kwa maringo;tena beberu;na mfalme mbele ya watu wake.

32. Kama umekuwa mpumbavu hata ukajisifu,au kama umekuwa unapanga maovu,chunga mdomo wako.

33. Maana ukisukasuka maziwa utapata siagi,ukimpiga mtu pua atatoka damu;kadhalika kuchochea hasira huleta ugomvi.

Methali 30