18. Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu,naam, mambo manne nisiyoyaelewa:
19. Njia ya tai angani,njia ya nyoka mwambani,njia ya meli baharini,na kinachomvuta mwanamume kwa mwanamke.
20. Mwenendo wa mwanamke mwasherati ni hivi:Yeye hula, akajipangusa mdomo,na kusema, “Sijafanya kosa lolote!”
21. Kuna mambo matatu ambayo huitetemesha dunia,naam, mambo manne ambayo haiwezi kuyastahimili:
22. Mtumwa anayekuwa mfalme;mpumbavu anayeshiba chakula;
23. mwanamke asiyependwa anayeolewa;na mjakazi achukuapo nafasi ya bibi yake.
24. Kuna viumbe vinne vidogo sana duniani,lakini vina akili sana:
25. Sisimizi: Wadudu wasio na nguvu,lakini hujihifadhia chakula wakati wa kiangazi;
26. pelele: Wanyama wasio na uwezo,lakini hujitengenezea makao miambani;
27. nzige: Hawana mfalme,lakini wote huenda pamoja kwa vikosi;
28. mjusi: Waweza kumshika mkononi,lakini huingia katika ikulu.
29. Kuna viumbe vitatu vyenye mwendo wa kupendeza,naam, kuna viumbe vinne vyenye mwendo mzuri;
30. simba: Mnyama mwenye nguvu kuliko wote,wala hamwogopi mnyama mwingine yeyote;