31. Usimwonee wivu mtu mkatili,wala usiige mwenendo wake.
32. Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu;lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.
33. Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu,lakini huyabariki makao ya waadilifu.
34. Yeye huwadharau wenye dharau,lakini huwafadhili wanyenyekevu.
35. Wenye hekima watavuna heshima,lakini wapumbavu watapata fedheha.