Methali 3:3-15 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Utii na uaminifu visitengane nawe.Vifunge shingoni mwako;viandike moyoni mwako.

4. Hivyo utakubalika na kusifika,mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu.

5. Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote,wala usitegemee akili zako mwenyewe.

6. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo,naye atazinyosha njia zako.

7. Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima;mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.

8. Hiyo itakuwa dawa mwilini mwako,na kiburudisho mifupani mwako.

9. Mheshimu Mwenyezi-Mungu kwa mali yako,na kwa malimbuko ya mazao yako yote.

10. Hapo ghala zako zitajaa nafaka,na mapipa yako yatafurika divai mpya.

11. Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu,wala usiudhike kwa maonyo yake;

12. maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye,kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi.

13. Heri mtu anayegundua hekima,mtu yule anayepata ufahamu.

14. Hekima ni bora kuliko fedha,ina faida kuliko dhahabu.

15. Hekima ina thamani kuliko johari,hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo.

Methali 3