Methali 3:20-27 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka,na mawingu yakadondosha umande.

21. Mwanangu, zingatia hekima safi na busara;usiviache vitoweke machoni pako,

22. navyo vitakuwa uhai nafsini mwako,na pambo zuri shingoni mwako.

23. Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama,wala mguu wako hautajikwaa.

24. Ukiketi hutakuwa na hofu;ukilala utapata usingizi mtamu.

25. Usiogope juu ya tishio la ghafla,wala shambulio kutoka kwa waovu,

26. Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza;atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.

27. Usimnyime mtu anayehitaji msaada,ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo.

Methali 3