9. Mwenye hekima akibishana na mpumbavu,mpumbavu huwaka hasira na kucheka bila kutulia.
10. Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia,lakini watu wema huyalinda maisha yake.
11. Mpumbavu huonesha hasira yake wazi,lakini mwenye hekima huizuia na kuituliza.
12. Mtawala akisikiliza mambo ya uongo,maofisa wake wote watakuwa waovu.
13. Maskini na mkandamizaji wanafanana kwa kitu kimoja:Wote wawili wamepewa macho na Mwenyezi-Mungu.
14. Mfalme anayewaamua maskini kwa haki,atauona utawala wake umeimarika milele.
15. Adhabu na maonyo huleta hekima,lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake.
16. Waovu wakitawala maovu huongezeka,lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao.
17. Mpe nidhamu mwanao naye hatakupa wasiwasi;yeye ataufurahisha moyo wako.
18. Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu;heri mtu yule anayeshika sheria.
19. Mtumwa haonyeki kwa maneno matupu,maana ingawa anayaelewa yeye hatayatii.
20. Wamwona mtu apayukaye bila kufikiri?Mtu mpumbavu ni afadhali kuliko yeye.
21. Ambembelezaye mtumwa wake tangu utoto,mwishowe mtumwa huyo atamrithi.