Methali 29:21-27 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Ambembelezaye mtumwa wake tangu utoto,mwishowe mtumwa huyo atamrithi.

22. Mwenye ghadhabu huchochea ugomvi,mtu wa hasira husababisha makosa mengi.

23. Kiburi cha mtu humporomosha mwenyewe,lakini mnyenyekevu wa roho atapata heshima.

24. Anayeshirikiana na mwizi anajidhuru mwenyewe;husikia laana ya aliyeonewa bila kusema neno.

25. Kuwaogopa watu ni kujitega mwenyewe,lakini anayemtumaini Mwenyezi-Mungu yu salama.

26. Wengi hupenda kujipendekeza kwa mtawala,hali mtu hupata haki yake kwa Mwenyezi-Mungu.

27. Mdhalimu ni chukizo kwa mnyofu,naye mnyofu ni chukizo kwa mwovu.

Methali 29