2. Taifa la fujo huzusha viongozi wengi,lakini kwa kiongozi mmoja mwenye akili na maarifa huwa na utengemano
3. Mtu mhitaji anayewadhulumu maskini,amefanana na mvua kubwa inayoharibu mimea.
4. Watu wanaovunja sheria huwasifu waovu,lakini wanaoishika sheria hupingana nao.
5. Waovu hawajui maana ya haki,lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa.